JAMANI SERIKALI YA MKAPA INATUPELEKA WAPI?

Moderator:Juma4admin

sedon_jr
Junior Member
Posts:9
Joined:Fri Sep 06, 2002 1:42 pm
Contact:

Fri Sep 06, 2002 9:33 pm

Hivi jamani hawa jamaa tukishawachagua mbona wanatupeleka wanavyotaka wao?Yaani inafikia wakati inakuwa too much.

Hapo nyuma nilipokuwa nikiona masela wanatimkia majuu niliona kama si wazalendo ila sasa nimeanza kuelewa.

Labda twende na fact kabisa.Mheshimiwa sana Mungai kwa nguvu zote alitangaza kuwa mwanafunzi atakayepata division 4 kidato cha nne au sita hatapata cheti ng'o.Ukiangalia kwa harakaharaka utaona hii ni shega tu lakini hebu jiulize ni kipi hawa jamaa wamewasaidia watahiniwa hawa wasipate hizo division 4 kama sio kila siku kuwabana?Mara vitabu hamna,mara walimu hamna, mara michango isiyokuwa na kichwa wala miguu[nasikia juzijuzi hapa wanafunzi Bongo wamechangishwa mchango wa mbio za fimbo za malkia wa uingereza!],mara format za mitihani zinabadilishwa,mara vitabu vya kujibia mitihani vinabadilishwa kiholela,yaani ilimradi ni vurugu tupu.Bado unakuwa na nguvu ya kumyima mtoto wa watu cheti?Kwanza zaidi ya robo ya watahiniwa wanapata div.4 na zero!Tafuteni njia za kuwasaidia sio kuwabania

Acha hilo sasa wamekuja na mpya.Eti washikaji wamejipinda wakapata divisheni zao kali tu zinazowapa kila haki ya kulipiwa na serikali[Tena majina yao yametoka ktk orodha ya waliochaguliwa na chuo kikuu] serikali inawaambia HATUNA PESA,TAFUTENI WADHAMINI BINAFSI.Jamani huu sio ugaidi?Hivi kodi za watanzania zinaenda wapi?Hivi pesa ya kununulia rada inayowafanya hata waliyoitengeneza watushangae zinatoka wapi?Hivi kuna umuhimu gani wa kununua ndege ya raisi wa bongo ya gharama ya ajabu na kuwaacha watoto wa walipa kodi[waliofaulu katika mazingira magumu/kwa juhudi zao]wakiwa mtaani bila la kufanya?

Mi nasema huu ni ugaidi.Vitendo vya utapeli na ujambazi vikiongezeka nani alaumiwe.Yes kwa sababu vijana hawa hawana cha kufanya!Nani leo hii atakuajiri na form six yako?

Kweli bongo kuna amani,oh samahani,utulivu[amani itoke wapi usawa huu]Ingekuwa mambo haya yametokea hapo jirani tu kwa baba Moi niambie nini kingetokea?Hapa ndipo ninapomkumbuka Mwalimu Nyerere.Sidhani kama angevumilia kuona vijana hawa wakigaidiwa kiasi hiki.

Mimi binafsi sijasoma ila naona uchungu kuona washikaji wakigaidiwa nchini kwao. :?
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 3 guests