UVAAJI WA KUIGA MAREKANI UNAWAKILISHA ??? (KEEPIN IT REAL?)

Moderator:Juma4admin

sedon_jr
Junior Member
Posts:9
Joined:Fri Sep 06, 2002 1:42 pm
Contact:

Sat Sep 07, 2002 12:17 pm

Sasa Mkuki nashukuru umeanza kuingia pale panapotakiwa.Hayo mawazo ya kufikirika ni mazuri,tena mazuri sana ila ukweli unabakia palepale kwamba hayawezi kutekelezeka bila kuwepo na uhalisia.Mifano ya mapinduzi ya China,Uingereza na kwingineko naomba uitathmini kwanza halafu uone kama hautakubaliana na mimi.Unajua kwanini?Wao walianzia kutazama mbali:kung'oa tatizo tokea kwenye mizizi[sisi mizizi ya tatizo letu ni uchumi]Hatuwezi kufanya chochote tukakiita mapinduzi kama uchumi wetu utaendelea kuwa ulivyo sasa.Narudia tena.Nani atakayeacha kununua mitumba ambayo unaipata kwa shilingi 100 aende kuutukuza utamaduni wakati hana uhakika wa kula siku inayofuata?

Mimi ningefurahi kama mngewapigia kelele hawa jamaa wanaogawana kodi yetu kwa kujinunulia mashangingi na ndege za gharama,pamoja na rada ambayo matumizi yake hayako tanzania.We Mkuki hebu angalia hao wabunifu wa mavazi watatoa wapi malighafi wakati viwanda vyote vya bongo vinauzwa kwa wageni kama sio kufungwa kabisa.Unategemea mchina aje autukuze utamaduni wako?

Juzijuzi tu hapa wasauzi "walopewa" kiwanda cha bia walikuwa manataka kutikisa kiberiti.Eti wanataka walete shayiri toka kwao kuja kutengenezea bia bongo.Tanzanite inachimbwa Bongo lakini Kenya wamezawadiwa boeing kwa kuwa wazalishaji wazuri wa Tanzanite,Kwa mtaji huu kwa nini msiwabane kwanza hawa jamaa waturekebishie maswala ya uchumi?kwasababu tukiwa fit kwenye mambo ya uchumi tunaweza kuanza kuongelea maswala hayo ambayo kwasasa ni ya kufikirika tu.Bado naheshimu sana mawazo yenu.
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Sat Sep 07, 2002 7:37 pm

Nakubaliana na wewe Sedon kuwa uchumi unaturudisha nyuma katika mambo mengi lakini hata hivyo mimi nafikiria pia na attitude yetu huwa inachangia. Halafu sababu ya kutoanza kulaumiana na viongozi ni kuwa kwanza topic yenyewe haihusu hayo uliyoyasema (ingawa pia ni vizuri kuyaangilia maana ya affect tunachokiongelea) ninasema hivi ili tubaki ndani ya topiki kwa sababu tutajikuta hatuongelei tena kuhusu wasanii wetu kuwakilisha na kujikuta tuonaongelea uhalali wa kununua rada,kodi na mambo mengineyo ambayo nadhani yanahitaji kufunguliwa topiki yake yenyewe kabisaa!

Mimi kuna kitu kimoja huwa kinanisumbua kuhusu sisi waafrika nacho ni organization mimi nadhani hili ni tatizo letu kubwa kuliko hata hao viongozi (ingawa sifikiri viongozi wote ni wabovu) sisi kila siku tumekalia serikali hivi serikali vile...sasa hebu tujiulize kwa dk moja...je ni nini ambacho sisi tunafanya kwa nchi zetu/bara letu?Sio siye ambao tunakaa maofisini tunapiga soga siku nzima?sasa hapo nani alaumiwe serikali?Sio sisi ambao asilimia zaidi ya hamsini ya wenye uwezo wa kuzalisha hatuzalishi?(nikimaanisha productive population) Tumekaa tu kulalamika ajira ajira serikali hizo ajira itazitoa wapi kama uchumi wote kwa ujumla uko chini?Mimi huwa najiuliza hivi wasomi wanne waliomaliza digrii zao UDSM katika nyanja tofauti kwa mfano mchumi, business administration, sheria, na engineer au labda computer scientist hivi hawa hawawezi ku network wakajiajiri wenyewe?nikimaanisha hawa ni watu waliosoma lakini wao wanafikiria kuajiriwa...nchi hizo zilizoendelea ni sekta binafsi ndio inayoajiri watu wengi zaidi na sio serikali na hata marekani yenyewe ina tatizo la unemloyment. Hao jamaa wanaweza kuanzisha biashara yenye mafanikio kabisa kutokana na ujuzi wao na kwa sababu wamesoma wanaweza kuwa na proposal nzuri ya kupata mikopo au sponsors kutoka hata nje ya nchi kwa ajili ya kuanzia. Sasa fikiria tunge create ajira kwa watu wangapi kama wengi wangefanya hivyo? Vitu vingine ni sisi wenyewe tu kubadilisha jinsi tunavyofikiri maana kama umeona serikali haikusaidii unafanya nini kujisaidia mwenyewe? Tumekaa lawama tu wakati unasikia "duh jamaa alikuwa meneja lakini katoka kabwela tu wala hajaiba, kweli huyo mpumbavu" sasa kwa attitude hiyo ya nikiingia lazima niibe je kweli uchumi utakua? Kungekuwa na uwezo wa kukusanya takwimu mimi nina uhakika kabisa kuwa raia wana more to blame kwa sababu na wao washaamua kutosaidia chochote! Kama baba yako kaamua kuto provide home wewe utakaa tu ufe njaa au utaangalia njia ambayo unaweza ku generate income ili usaidie na wadogo zako? kama utakaa tu ulaumu basi utakuwa mwendawazimu na utakula lawama zako!Hakuna nchi ambayo viongozi hawaibi bwana tofauti ni kuwa kuna nchi ambazo raia wanafanya kazi (na Tanzania sio mojawapo!) na hii ndio haswa sababu ya mimi kutokaa nalaumu serikali maana najua haitabadili kitu!Wewe jiulize kwa nini vijana kibao wabongo wanaondoka nchini wanaenda kusoma nje halafu hawataki kurudi nyumbani. Kinachoniudhi ni kuwa hawa ndio wamekalia lawama tele ooh bongo hivi bongo vile! mimi nawauliza wewe na PHD yako ya political science unafanya nini huku marekani kama una uchungu si uende ukagombee uongozi basi ili ulete hayo mabadiliko unayoyataka? Hii ni typical attitude ya immigrants na inanichefua kishenzi kwa sababu ni hao hao wanafiki ambao hawana huruma kwa ndugu zao kwa sababu wao sasa hivi wanapulizwa na kiyoyozi na ameoa mzungu basi amekalia kulaumu tu wakati yeye ndio yuko kwenye position nzuri ya kuleta mabadiliko!Sasa mimi nauliza nani alaumiwe? nchi bila nguvu kazi hata ingekuwa na uongozi bora vipi bado ingekuwa masikini?labda iwe ya kidikteta ambapo watu wanafanyishwa kazi kwa mtutu wa bunduki!think about it!

Sedon unaona jinsi tunavyoenda nje ya topiki? Anyway turudi kwenye hoja au tuanzishe nyingine kwa ajili ya majadiliano haya tu maana bodi yenyewe hii ya HipHop tusije kuwaboa watu hapa!mida!
sedon_jr
Junior Member
Posts:9
Joined:Fri Sep 06, 2002 1:42 pm
Contact:

Sun Sep 08, 2002 8:09 pm

nimekufahamu mkuki.Ok tutaiongelea hii hoja vizuri ktk mada ambayo itakuwa inaendana nayo.Naheshimu mawazo yako.
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Thu Sep 12, 2002 10:43 pm

Soul cheki profile yangu utakuta e mail hapo hapa nimeiona soo kuiweka maana watu wa junk mails huwa wanatumia vi script fulani ku collect e mail za watu kwenye mitandao kwa hiyo si unaelewa mwenyewe mambo ya kubadilisha address kila siku soo! Ndondoshee line tu hapo nitakujibu!

Ebwana Guest noma namna hiyo mwanangu sign up basi na handle yako ili tujue wewe nani maana tayari ushakuwa mwenyeji au sio!?

Ebwana unachosema kuwa hiphop ni utamaduni wala hujakosea kabisa unajuwa tatizo linakuja wapi? tena mwenyewe umesema...tatizo liko kwenye kuiga...na mimi tatizo haswa sio kuiga nguo za nje bali tatizo langu ni kuwa tunalemaza "fashion industry" yetu kitu ambacho kwa umaarufu wa nyimbo za kwetu sasa hivi (mf:Bongo HipHop) kingekuwa kinasadia kuleta ajira kwa wanaobuni mitindo na kadhalika. Hiyo ni tukiacha swala la kujivunia utamaduni wetu; hapo tunaongelea tu katika upande wa kibiashara, mimi naamini Hiphop ya bongo kwa jinsi inavyoinukia kwa kasi ita create a whole new economy in itself kama vile Hiphop industry ya marekani. Kinachoifanya Hiphop industry ya Marekani iwe a multibillion dollar enterprise ni kwa sababu hela inazunguka ndani kwa ndani, yaani wao ndio wanatengeneza bidhaa hiyo na tayari wana soko zuri ndani ya nchi yao bila kusahau soko lao la nje ya nchi ambalo na siye wavaa FUBU tunasaidia kuliendeleza!Mimi nadhani kama tungeweza ku glorify utamaduni wetu hata kama ungekuwa modernized lakini kiini chake bado kiwe chetu; in time tungeweza ku create market ya bidhaa zetu humo humo nchini mwetu na bara letu kwa ujumla!Si wanasema charity begins at home? Mimi nadhani mtu unaweza kuwakilisha bila kuvaa rubega...nilitoa mfano awali kama mimi binafsi nina rock shati langu la kiafrika na jeans labda na raba, buti au sandals hapo tayari nishawakilisha. Badala ya kuvaa cheni ya bling bling yenye "ice" ambazo zinawaua waafrika wenzangu huko Angola,Sierra Leone,Liberia na kadhalika ninatinga Neclace yangu ya kitamaduni labda na shaba au mbao, au mfupa uliochongwa vizuri. Huu ni wakati ambao sisi kama watu weusi tuanze kubadili fikra zetu...hizi dhahabu na almasi kama nilivyosema awali zinasaidia kuwaua ndugu zetu Afrika, haya mavazi tunayonunua na huu uchumi wa hawa watu ambao tunausukuma kwa jasho letu na vijisenti vyetu vya ngama ndio huo huo unaotumika ku develop silaha za kisasa zaidi ambazo ndio zinatumika kutukandamiza ili tusiwe na sauti!Watu wanasema hizi siasa kumbe ndio reality yenyewe utajiri wa nchi za magharibi unachangiwa na sisi vilevile kuanzia katika kuwapatia soko hadi katika kuwapatia malighafi...haya nini ambacho wao wanaturudishia? Nada...sana sana wanachotuletea sisi ni matatizo tu na vita kila kona ya bara letu, magonjwa ya kila aina na madhila mengine kedekede...now how is this related to HipHop? Angalia HipHop iliyojaa redioni na HipHop isiyopigwa maredioni na kwenye Televisheni utaniambia kama sio siasa!HipHop ilitupa sauti sisi watu weusi ya kuweza kusema matatizo yetu hence the fact kuwa hiphop ni way of life; lakini ni nini sasa HipHop maisntream inawakilisha? Bling Bling, kukandamiza wanawake na violence...je kweli hiyo ni sauti ya watu wa chini? Nani yuko responsible? Hivi ni vijiswali tu!

Anyway mshkaji ulikuwa unauilizia wapi utapata gear zinazowakilisha ki home! mimi huwa navuta nguo pale mwenge kwenye duka la Afrikasana hawa jamaa kwa kweli wako fiti sio vi batik vya kichovu hawa nguo zao zinawakilisha kweli sanaa...sehemu nyingine ni nyumba ya sanaa ingawa hawa inabidi na wewe uwe na taste nzuri maana kuna nyingine kidogo michosho ila na wao wanajitahidi kuwakilisha!wewe saka saka pale bongo vitu kibao tu!Halafu kama uko nje ya nchi au kama unaweza kutuma vitu mtandaoni kuna site nitakuja kuziweka hapa nimezi bookmark!vitu kutoka Afrika Magharibi (hawa jamaa nguo zao bomba mbaya lazima tukubali!) afrika kaskazini na sehemu nyingine mbali mbali.

Oya mida masela...
soulrebel
Junior Member
Posts:6
Joined:Fri Sep 13, 2002 10:56 am
Contact:

Fri Sep 13, 2002 11:09 am

nilikua sina uhakika kama nimesign ndani, lakini profile yako mk haina email adress yako, nadhani unafahmu hilo fika, eneway chek yangu
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Sat Sep 14, 2002 12:08 am

Ebwana Soul Sorry unajua nilikuwa nimesahau kuwa nilikuwa nimechagua address yangu isiwe public...sasa hivi nisharekebisha kwa hiyo shega!Ebwana yako naona nayo rhumba hilo hilo nayo iko hidden anyway yangu sasa hivi iko public kwa hiyo we nicheki tu kiaina kwenye hiyo anuani!
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Sun Sep 15, 2002 5:45 am

Ebwana Guest nakubaliana na wewe kuwa kuvaa ni element moja ya HipHop ingawa nitakwambia kabisa kuwa hilo swala ambalo ni pana sana kwa mfano! Miaka ya mwanzo ya HipHop uvaaji haukuwa sawa na wa sasa hivi!Fashion zinabadilika...kuna wakati fulani Afrocentrism na HipHop vilikuwa vinaenda bega kwa bega kama utakumbuka video za zamani watu kibao walikuwa wanavaa zile medals za kiafrika zenye ramani ya afrika na kadhalika na hata batik (ambazo marekani wanaita daishiki!) zilikuwa zinatingwa kwa sana tu sasa kama unataka kuongelea swala la mavazi nadhani Nguo za kiafrika basi zinawakilisha kwa sana tu...halafu usisahau HipHop ni sanaa ya watu weusi na katika HipHop hamna aina ya mtindo ambayo ndio imekuwa defined kuwakilisha hiphop!Kama unafahamu naomba unipe mifano (badala ya baggy jeans na Tshirt au Majacket!) Kama utakuwa una observe vizuri utakuta hata ma jacket yanavaliwa wakati wa baridi kwa mfano southern HipHop huoni sana majacket lakini ukiangalia East Coast HipHop kwa mfano utaona majacket ni hooded sweatshirts zinaonekana zaidi. Angalia usije ukawa unasahau kuwa HipHop ya Marekani inaendana na Coast...kuanzia beats, rhymes mpaka mavazi sasa sijui wee unaangalia hiphop ya wapi...ndio maana nikakwambia ni ngumu sana kusema haswa mavazi gani ndio ya HipHop.

Sasa tuende kwenye nilichotaka kuongelea; nilikuwa nataka kukukumbusha kuwa hapa tunaongelea African HipHop (rejea jina la website!) na hususana Tanzanian HipHop (bongo flava) sasa kama tushaamua kuimba kwa kiswahili ili kuwakilisha home sasa wewe huoni kuwa na mavazi yakiendana na home ndio tunawakilisha ipasavyo? Tukiangalia tena jinsi ulivyoongelea kuhusu mavazi ni kuwakilisha je ulikuwa unamaanisha basi hata ku rap iwe ni kwa kiingereza au maana ndio hiphop ilivyoanza si ndio? Sasa hapo tutakuwa tunamuwakilisha nani?

Hilo swala la HipHop as a culture tushaliongelea na hamna anayepinga labda ungesoma post zilizopita ungegundua kuwa tumekubali hilo!Lakini kumbuka kuwa na Tanzanian HipHop is a culture also na ndio maana kuvaa kiafrika kwa mtazamo wangu ingekuwa inawakilisha zaidi!

Lakini mshkaji ninakubaliana na wewe kuwa kuvaa ni element mojawapo ya hiphop ila pia inabidi tujiulize kuwa je element ya Tanzanian HipHop ni nini?Je Ni Phat farm (classic American flava kama slogan yao inavyosema!), Sean John, PelePele n.k?

Mwisho nilikuwa nataka kusema tu kuwa haya ni majadiliano tu sio criticism ya aina yoyote swala la kuvaa ni swala la uamuzi wa mtu ila nadhani watu hapa wanatoa mitazamo yao tu juu ya swala hili...amani!
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 3 guests