UVAAJI WA KUIGA MAREKANI UNAWAKILISHA ??? (KEEPIN IT REAL?)

Moderator:Juma4admin

bongonian
Junior Member
Posts:15
Joined:Sat Nov 03, 2001 8:01 am
Contact:

Tue Sep 03, 2002 7:21 am

yaani mnachosema soulrebel na mkuki ni sawa kabisa......

kwanza kabisa solrebel ..brainwashed =kupumbazwa,kutiwa changa la jicho

nina mchango mmoja ...tunafahamu wabunifu wa mavazi bongo wapo lakini kuna kitu kinachonishangaza ni kwanini nguo zile za asili(batiki) zinashindana na designers labels...maana yangu ni kuwa unaenda kuangalia nguo ya kha....(sitaji jina) unakuta bei yake ni karibu na FUBU iliyotundikwa dukani sasa kwa hali kama hii situtakuwa tunajiwekea ugumu wenyewe.

lakini kuna kitu nilifikiria juzi baada ya kusikia habari za cool james..nikasema ni bahati mbaya jamaa kavuta lakini wasanii wa kibongo watachukulia kama changamoto kwa kuendeleza maendeleo yao wenyewe...kwa mfano wakikaa chini wajaribu kujadili fainali ya bongo flavor watajua nini kinahitajika kufika huko ng'ambo na labda wataweza kufikiria hata swala la vazi la asili.
Mchapakazi
Member
Posts:86
Joined:Thu Mar 01, 2001 8:01 am
Contact:

Tue Sep 03, 2002 12:41 pm

Mkuki, Soul Rebel Mmebainisha yote lakini tatizo ni kwamba waelewa wachache plus emecee wengi awatii timu huku tunataka kusikia maoni yao pia namean? Bongonian mambo ni aje za siku ndugu yangu nimekuwa nikiangaika huku na kule na pc yangu naiona mbali kidogo ni kweli jamaani watu lazima wabadilike walikuwa hawasikilizi sasa wanasikiliza na kununua tuwaamishe na kwenye mavazi basi tujuvunie fahari yetu ingawa hata vazi la taifa atulijui lakini batki imepata chati flani inaweza kuwa hivyo ingwa sio official vazi la taifa labda khanga! aiight mida
bongonian
Junior Member
Posts:15
Joined:Sat Nov 03, 2001 8:01 am
Contact:

Tue Sep 03, 2002 8:15 pm

vipi mchapakazi..kwanza j4 kafungua uwanja wa vita umeuona? nilitegemea ile vita ya tmk na kino itarudishwa.

hii forum naona mkuki na solrebel wamemaliza kuelimisha jamii isipokuwa wale wanaodhania vazi letu noma wanaweza kuangalia topic ya "je watanzania tuna vazi la asili" nadhani watu walijadili sana hili swala la uvaaji
mimi binafsi asilimia themanini ya mavazi yangu ni batik...nazuka disco,shule, na sehemu yoyote ile na wala sijali na ninajisikia vizuri sana!kwa hiyo personally I talk the talk and walk the walk ingawa mimi sio msanii!
hongera sana mkuki kwani wengi wamejaribu lakini wameshindwa
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Wed Sep 04, 2002 6:28 pm

Sawa sawa wazee...mimi kwa mtazamo wangu nadhani swala la vazi la kitaifa ingawa ni muhimu lakini kutokuwa na vazi la taifa sidhani kama ndio kigezo cha kutufanya tusivae nguo za kiafrika!

Lazima tuelewe kuwa tanzania ukiangalia swala la makabila ni "very diverse" yaani tuna mavazi ya aina nyingi sana...sasa mimi kama ningekuwa designer wa nguo za kiafrika ningefanya research ya nguo zinazovaliwa katika makabila tofauti ya Tanzania halafu ninge combine elements tofauti za mavazi hayo na ningetoka na kitu kikali ambacho kinawakilisha hiyo diversity yetu watzanzania. Ningekuwa waziri wa Utamaduni ningeandaa shindano kubwa la nchi nzima kwa madesigner wa Tanzania kudesign (jamani samahanini hivi design kwa kiswahili ni nini maana naona ishakuwa taabu!...ndio mambo ya kasumba haya!) vazi rasmi la Taifa la wanawake na wanaume ambalo litatumika hata na viongozi kutuwakilisha (angalia wenzetu wa afrika magharibi haswa NIgeria) wale washindi watatu wa juu watakaa pamoja na ku design sasa final national attire. Huu nadhani haswa ni mzigo wa Wizara ya Utamaduni lakini kwa sababu najua kutegemea hawa mabwana wakubwa kuitufanyia kazi haitufikishi kokote ni wajibu wetu kuwakilisha kwa jinsi tunavyoona itafaa...mimi nadhani batik,mashati ya vikoi yanawakilisha kinoma tu hata kama hujatinga full suit lakini walau shati na jeans haina noma wala nini nakumbuka kama mara mbili niliona hard blasters wamepanda kwenye steji na batik enzi zile chemsha bongo imetoka tu!lakini sijui kama bado wanaendelea maana mimi niko mbali na home!

Kuhusu swala la vyombo vya habari ingawa nakubali kuwa wana reflect kitu watu wanachopenda nadhani ukiangalia sana utakuta wao ndio wanaochagua nini watu wapende...yaani wao ndio wana influence public opinion; na hii ni charactreristic ya vyombo vya habari vinavyioendeshwa kwa matangazo (commercial media) kwa sababu wao wanapangiwa na wafadhili wao...kwa mfano kama matangazo ya bia na sigara yaakuwa mengi kwenye TV ukifanya research utagundua kuwa mauzo ya vitu hivyo viwili yamepanda, na dnio maana unaona wanaendelea kutangaza maana wanatengeneza hela...nadhani tukiangalia cause and effect utakuta media inaanza ndio watu wanafuatia...since tuko kwenye hiphop tuangalie mfano huu: HipHop ya bongo ilianza vipi kukubalika kwa watanzania wali wengi yaani mainstream Tanzanians? ni baada ya nyimbo kuanza kupata more airplay katika vyombo vya habari tofauti na zamani ingawa kuna sababu nyingine kama ubora wa production lakini mimi naamini hiyo ndio ilikuwa sababu kuu. Kama ulikuwa unafuatilia historia ya hiphop bongo zamani ulikuwa muziki wa washamba (mabitozi walivyokuwa wanuona) lakini sasa hivi hata disko unapigwa na watu wanajirusha...mimi nakumbuka kuna wakati mmoja nilikuwa bills ukapigwa wimbo wa Hashim - shadows of a dark destiny kama sikosei watu wote wakaondoka kwenye sakafu ya kuchezea na hii sio mara moja tu mara kadhaa yaani hadi DJ inabidi autoe chapchap!Ukiangalia utakuta watu walianza kuusikia muziki huu redioni na sasa hivi unaona kuwa hadi mauzo ya kanda yamekuwa makubwa kishenzi na mpaka unaona na mamcee wameongezeka pia, na kali ka myth kuwa ni muziki wa kihuni kameanza kupungua pungua ingawa kuna wachache ambao bado wanawakilisha hiyo fikra kwa kukosa rhymes zilizo makini!

Kama hii leo media inge glorify utamaduni wetu na wakawa consistent na hilo yaani wao kila siku bango...polepole ungeona ma mcee na wanaanza kutinga mapigo ya kiafrika na mwishowe kutoka hapo unakuta na washabiki (ambao ndio sie tulio wengi) tunaanza kutinga hivyo hivyo..ukicheki utaona zamani bongo flava kama nilivyosema awali ilikuwa ya wachache tu...lakini utakuta siku hizi hata matozi wa uzunguni (ambao wengi ndio malimbukeni wanaodandia tu bila kujua undani wa kitu) nao wameanza kuusikiliza...yaani siku hizi "maisha ya uswazi" baada ya gangwe yamekuwa dili watu wanaona ujanja kujiita mtoto wa uswazi wakati zamani ilikuwa aibu...feel me!?

Jamani mida naona lishakuwa gazeti hili tena!lakini wazee pointi nzuri sana najifunza mengi kutoka kwenu :)
sedon_jr
Junior Member
Posts:9
Joined:Fri Sep 06, 2002 1:42 pm
Contact:

Fri Sep 06, 2002 8:23 pm

Washikaji mi naona tuongee vitu ambavyo vipo,si vya kufikirika yaani tuongee vitu ambavyo hata mwenyewe ukikaa chini ukatafakari utaona vinaelekea kwenye mstari.

Sisemi hivi kwamba nayaponda mawazo yenu,hapana.Hapo tuelewane kwanza,ila ninachosema mimi ni kuwa nyinyi mmeelemea zaidi kwenye mawazo ya kufikirika zaidi kuliko kutekelezeka.

Kwa nchi kama Tanzania naomba msahau kabisa kitu kinachoitwa vazi la Taifa hata kama itapita miaka mingapi.We angalia tunasema tuna lugha ya Taifa tangu Mwalimu anaitawala nci hii lakini tizama mtiririko wa mawazo ya mheshimiwa Mkuki uniambie ni lugha gani kama si kiswanglish?Hapo ndipo tunaporudi palepale.Kama Kiswahili tumeanza nacho tangu miaka ya 1960' na bado sisi tunaojiita waswahili hatuongei kiswahili wapi litawezekana vazi la Kitanzania?

Nikienda moja kwa moja kwenye mada ni kuwa hili jambo linakuwa gumu kwa sababu mbalimbali ingawa mi nitawapa mbili kwa leo.Kwanza umasikini.Kila siku maburungutu ya mitumba tena kwa bei bwerere yanaingia nchini halafu umwambie mtu akavae bazee au batiki ambayo kabla hajaweka gharama za mashono anaweza akapata mitumba gunia mbili!Pamba za kibongo tukubali tukatae ni gharama kuliko mitumba tuliyoizoea.

Pili ni historia.Mshikaji wangu soulrebel mwenyewe ushalikubali hili halafu tena ukatoka nje!Wazungu walishatuwekea umimi.achilia mbali ile kusema mmasai yuko bongo na kenya na mngoni kuwako tz na bondeni.Ila kuna hili lamwalimu kutuchanganya wabongo hadi kushindwa kusema mi mmasai bwana!au mi mbondei kwani kila mtanzania anaishi sehemu yoyote ya bongo anayotaka yeye.Sasa niambie tuvae rubega za wamasai,mgolole wa wagogo au mashuka ya wambulu?

Tukubaliane tu kwamba kwa hali halisi iliyoko kuwako kwa vazi la kitazania au la kiafrika ndani ya nchi kama tanzania ni ndoto za alinacha.Ngoja niishie hapa kwa leo
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Sat Sep 07, 2002 2:51 am

Nimekufahamu mwanangu mwenyewe Sedon! Karibu barazani! Mimi nilikuwa naomba kutofautiana na wewe kidogo unapoongelea swala la mamab ya "kufikirika" kuna kitu kimoja unasahau ndugu yangu nacho ni kuwa bila hayo mambo ya kufikirika hakutakuwa na mambo ya kutekelezeka!yaani ni lazima watu tuumize kichwa kwa kupambanua mambo na kuja na mawazo mbalimbali ndipo tuone sasa ni vipi tutayakamilisha hayo mawazo yenyewe. Kitu kingine ambacho kinaturudisha nyuma waafrika ni hiki cha "haiwezekani" kama umesoma hoja ya awali ya Soulrebel aliongelea swala la mapinduzi ya kiutamaduni ya Uchina au kaangalie pia Iran n.k utaona kuwa swala la mapinduzi linawezekana, bila ya hivyo civil rights movement marekani isingekuwepo, utumwa usingeisha na mambo kibao ambayo yamebadilika yasingekuwepo maana ukiangalia wakati huo walikuwa wanaface force ya hali ya juu...kwa hiyo ndugu yangu hiyo attitude ya "haiwezekani" ndio haswa inayokushinda wewe mwenyewe.

Kuhusu swala la mimi kuchanganya kiingereza katika kiswahili changu utaona kuwa sehemu nyingi katika post zangu za awali nimeweka kwenye mabano kuwa ndio matokeo ya kasumba yaani mimi mwenyewe nimekubali kuwa siko nje ya kundi lililopumbazwa na hawa wazungu na hata mimi nina kazi kubwa ya kufanya hilo wala sikatai lakini walau ninajaribu kusafisha kichwa changu na wala sikai nikasema "haiwezekani"

Hilo swala la gharama za nguo ninakubaliana na wewe kuwa litaleta ugumu lakini hata hivyo mimi naamini kuwa ni kwa sababu hiyo hiyo ya kufuata fasheni za ulaya, kama ingekuwa sio hivyo nadhani pia ingesaidia yaani kama batik zingekuwa chati ingeleta tofauti fulani lakini tatizo ni kuwa watu hawazithamini na mtu anaona ni bora mtumba kwa sababu unaendana na fasheni za ulaya. Halafu hilo swala la makabila tofauti kama utakuwa umesoma hoja zilizopita utakuwa kuna mahali nimesema ma designer wanaweza kuja na mtindo ambao unachanganya mitindo ya makabila tofauti ili kuna na vazi ambalo linawakilisha zaidi makabila ya nyumbani!Hata hivyo hoja zako za msingi ila mwanangu mie sio mheshimiwa hicho sio cheo changu unaweza kuniita Mkuki tu inatosha!
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 4 guests