UVAAJI WA KUIGA MAREKANI UNAWAKILISHA ??? (KEEPIN IT REAL?)

Moderator:Juma4admin

Mchapakazi
Member
Posts:86
Joined:Thu Mar 01, 2001 8:01 am
Contact:

Tue Aug 27, 2002 1:27 pm

hEY What a topic! i like it ni kweli kabisaa je nani anawakilishwa eh maana afadhali basi label na studio zingekuwa na gear zao lakini nyingi bado well lakini zipo kama CBM Gangwe Gear najua wengine hawatavaa mtima huo lakini do these Guys produce enough collection kwa watu na wasanii? Well we can say Hiphop ni culture iliyoko world wide na inawakilishwa kwa mivaaji flani lakini inabidi kuangali mara 2 mbili aiight

Mida
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Thu Aug 29, 2002 12:04 am

Soul Rebel Topic ya maana sana umeanzisha!Big up!

Mimi kwa mtazamo wangu mavazi ya kiafrika yanawakilisha zaidi...nimekuwa napiga kelele kila siku kuwa dawa ni ku "stand out" kama tunataka kutambulika nje ya mipaka ya afrika mashariki ambako ndio kiswahili kinaeleweka zaidi na mojawapo ya njia ni kwa kuvaa tofauti na mainstream hiphop culture...jamani mtanisamehe kwa kuchanganya lugha ila ndio hayo hayo mambo ya kasumba mpaka tunajikuta lugha yetu wenyewe hatuwezi kuongea na kuandika kwa ufanisi...ngoja nirudi kenye topic...mimi sioni ubaya wa mavazi ya kiasili cha muhimu ni design na wala sio kitambaa gani kinatumika.

Hebu tuangalie hili swala katika mtazamo wa kiuchumi!

Tunaona kabisa kuwa Bongo Flava imekuwa maarufu sana nchini na kwa kiwango fulani inaanza kulipa yaani mauzo yanapanda siku hadi siku kutokana na ubora wa kazi yenyewe!Mimi nadhani hii imechangiwa na redio kuamua kuzipa kipaumbele bongo flava pamoja na studio kuboreshwa zaidi pointi ninayotaka kutengeneza hapa ni kuwa hili swala la kiuchumi linapatikana kutokana na collective effort na collaboration kati ya nyanja mbalimbali za sanaa husika yaani Hiphop inahusisha DJs,Producers,wasanii wenyewe pamoja na fashion...hiki ndio kinachofanya Hiphop ya marekani kuwa a multibillion dollar industry. Kila kitu kimeungana na kinaenda kwa networking nitakupa mfano katika mavazi hayo hayo "hiphop wear" Kina P Diddy na label yao wana endorse "Sean John" Kina Master P na No Limit wana endorse P. Miller Gear, Kina Jay-z na Rocawear, NAS na ESCO, Jeniffer Lopez na J-Lo na nyingine nyingi tu...utakuta kama mtu anamzimia sana Jay-z most likely atataka kuvaa kama yeye kitu ambacho kitamfanya akanunue nguo za Rocawear...hakuna tofauti kati ya hizi nguo ila ni majina ya designers tu na ukiangalia hawa wanamuziki sio designers wenyewe ila majina na umaarufu wao ndio unatumika hapa katika kuuza hivi vitu. Ninachotaka kusema ni kuwa kama tunataka kuzifanya nguo za kiafrika kuwa cool kama hizo Phat farm ni swala la wale watu ambao ni perceived as cool (wasanii) kuanza kuvaa nguo hizi...hapa utaona hata soko la nguo hizo linaanza kuinuka mwisho wa siku tunakuta katika kufanya hivi tunatengeneza industry yetu wenyewe na badala ya kuwatajirisha hao wamarekani ambao hata hawatujali tutakuwa tunabikisha hela zetu zina zikiwa zina circulate kwenye jumuia yetu wenyewe...hizo ni grassroots economics tu, tunalalamika hamna hela,ajira na vinginevyo wakati soko lipo ila siye tumelala tu!Hapa kuna soko la managers, critics, promoters,designers wa fashion, advertisers na mengineo...yote yanategemea sisi kama tunaweza kutangaza sanaa yetu na kuifanya ikubalike...na hivi ni kwa sisi wenyewe kuanza kuikubali!

Wewe Pampu mambo ya matusi ya kizamani sana mshkaji; kama huna hoja unaweza ukasoma tu ukaondoka sio lazima utukane watu...ustaarabu kitu cha bure tu!
hoya kama ni kuvaa ni kuva aunafanya sana kazi hili uishi sasa nini hata pamba usipige acheni mambo ya ulimbwende hayo hakuna cha kuiga ila ni kujipendezesha bye.
Chakubanga ni nini haswa kinazifanya hizo FUBU kuwa pamba na batik au nguo zozote za kiafrika kutokuwa pamba?Ndio hicho hicho nilichokiongelea hapo awali yote hiyo iko kichwani mwako tu hamna chochote special katika hizo nguo sana sana ni za bei mbaya tu wakati zinatengenezwa kwa fraction of what you pay![/quote]
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Fri Aug 30, 2002 5:58 am

Soulrebel Mwanangu yaani umegusia idara zote yaani inakuwa vigumu hata kuongezea...well presented!nimekupata!

Tatizo watu ukisema uliyoyasema wao wanasema unaleta siasa kwenye starehe, mimi nadhani hili ndio kosa kubwa sana kwa wengi wetu!kama tunavosema tunapigika lakini bahati mbaya hatujui nini kinachotupiga!Ukweli ni kuwa hii sio siasa bali ni hali halisi ya maisha na katika maisha kila kitu kinategemeana yaani ni kama mwili wa binaaamu ukikata kiungo chochote kile lazima mwili utaathirika kwa namna moja au nyingine hata kama utajifunza kuishi na ulemavu huo bado kutakuwa na shida fulani fulani...na tunachokifanya sasa hivi sisi watu weusi(wa marekani na wa barani Afrika) ni kukubali kuishi na huo ulemavu ndio maana hatuamki kubadili maisha tunayoishi nayo tunaishia kwenye icing lakini keki wanakula wengine!

Kama Soul utakuwa unafuatilia mjadala wa "reparations" kwa watu weusi utagundua kuwa mjadala mkubwa uko katika je malipo hayo yawe katika form gani?Kama ni fedha hawawezi kutulipa maana society zao ziko founded katika jasho la mtu mweusi na resources za bara letu kwa hiyo utakuta asilimia zaidi ya themanini inabidi waturudishie!Tatizo liko kwenye Madhara ya kisaikolojia...je hayo utayalipa vipi?

Niwape mfano...kulikuwa na poll moja miezi kadhaa nyuma katika bet.com ilikuwa inauliza je ukienda hospitali uko hoi karibu kufa ukakuta madaktari wawili, mmoja mweupe mwingine mweusi na wote wana kisomo sawa je utamchagua yupi akutibu ukizingatia wewe uko katika hali mbaya kwa hiyo unataka mtu aliye qualified enough!Asilimia zaidi ya 70 walisema kuwa watamchagua daktari mzungu, na usisahau bet.com ina mainly black audience sasa niambie ni kwa nini wameamua kumuamini mzungu zaidi ya mweusi mwenzao?Tunarudi pale pale soul alivyosema kuwa tumepumbazwa akili zetu kiasi cha kwamba hatuna sense of self worth tunapojilinganisha na hawa watu na ndio maana kila kitu chao tunaona kuwa ni bora zaidi ya chetu...si kila siku tunaona bongo akija mzungu hajasoma sana anapata kazi wakati mwafrika aliyempita kimasomo anaachwa!

Tujue kuwa tatizo hili hakuna wa kulitatua bali ni sisi wenyewe na njia ya kuanzia ni kuanza self purification na kuachana na kasumba zisizo na mpango...hapo juu kuna mshkaji kasema tunaosapoti hii ishu tungeanza kuvaa magome...unajua mshkaji kuna kitu kimoja unasahau...waafrika walikuwa wanavaa magome karne nyingi nyuma kwa hiyo hii leo huwezi kuvaa magome, jamii zina evolve tatizo ni kuwa wengi wetu kwa sababu ya kutojua historia yetu (mara nyingi ni kwa sababu historia yetu tumeandikiwa na mtu mwingine ambaye nia yake ilikuwa ni kuitumia kama chombo cha kututawala na kutuvua utambulisho wetu) Hili ni tatizo kubwa sana kwetu maana asiyejua anakotoka ni kama kipofu maana hawezi kujua anakokwenda na wala hawezi kujua makosa aliyofanya nyuma ili aweze kuyaepuka huko mbeleni!Kwa hiyo swala la magome hapa naona liko out of context ingawa kwa kweli kama liki designiwa fresh hilo vazi nalo linapendeza (usisahau haya magome huwa yanatengenezwa vizuri na yanakuwa kama kitambaa kabisa!) lakini mimi naona hilo vazi kwa sasa ni more ceremonial kuliko kuvaa kila wakati...mimi binafsi asilimia themanini ya mavazi yangu ni batik...nazuka disco,shule, na sehemu yoyote ile na wala sijali na ninajisikia vizuri sana!kwa hiyo personally I talk the talk and walk the walk ingawa mimi sio msanii!

Sio vibaya kuvaa hizo FUBU na kadhalika lakini mimi binafsi nilikuwa naona vizuri kwenye public places kama matamasha, kwenye interview za TV na Tours wangekuwa wanatinga kiafrika zaidi ingekuwa mwake yaani kama ku represent...mimi nadhani katika muda mfupi hata matozi slipway ungewaona wametwini batik...kama bongo flava ilivyoanza tu!matozi sa walikuwa wanaiona ya kishamba?mbona sasa wenyewe wanaenda kununua tape?Tatizo ni je hao wasanii wako tayari kufanya hivyo?Kama hiyo nukuu ya KRS ni kuwa Hiphop ni utamaduni rap ni kitu watu wanachofanya tu tatizo wasanii wengi na washabiki hawajajua kutofautisha hivyo vitu viwili!
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Sat Aug 31, 2002 8:04 am

Kizi nakupata mwanangu ni kweli unachoongea ila katika mabadiliko hayo japo yatakuwa ni ya muda mrefu nadhani ni lazima yaanzie mahali fulani...ninamaanisha kuwa kesho ni kesho tu hata siku moja haitafika...tunapoongea hapa sio siasa kama unavyosema bali ni hali halisi hata wewe ninaweza kutafsiri maneno yako kama siasa ni swala la unataka kuangalia majadiliano haya katika angle gani!

Mimi nakubali kuwa umaskini unachangia katika mambo mengi sana lakini vilevile ninadhani tatizo letu kubwa ni swala la kubadilisha mentality zetu!Mimi naamini tunaweza kutatua matatizo yetu bila msaada wa wageni tatizo ni je tunaamini hivyo?Je tunajiamini wenyewe?

Ninasema hivyo ili kutilia mkazo kuwa lazima tuanze sasa hii process hatuwezi kusubiri umasikini uondoke wakati hii yenyewe ni mojawapo ya njia za kupigana na umasikini kama mwenyewe ulivyosema kuwa uchumi na utamaduni ni vitu vinavyoshabihiana na mimi nakuunga mkono kabisa.Kwa mantiki hiyo basi ili uchumi uweze kukua basi inabidi na utamaduni wetu pia tuanze kuuenzi. Tatizo letu kubwa ni kuwa tuko so confused kiasi kuwa hatujui upi ni utamaduni wetu na upi ni wa kigeni; ndio tunarudi kulekule kwenye swala la mentality zetu!

Anyway naona tutaanza kutoka mbali na hiphop tuingie kwenye socio-economic issues hapa tusije kuwaboa watu wengine...lakini tusisahau kuwa hivi vitu vyote vinategemeana ndio maana ninasema kuwa siyo siasa bali ni ukweli wa maisha tu!
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 19 guests