EAST COAST TEAM KWELI TUTAFIKA

Moderator:Juma4admin

ODB
Junior Member
Posts:37
Joined:Fri Nov 23, 2001 8:01 am
Contact:

Thu Jul 10, 2003 10:28 am

Washikaji mi na wasi wasi kuhusu hii core inayojiita east coast team au watoto wa upanga.Wasiwasi wangu ni kutokana na team yao kuwapo ma presenter humo humo nao wanajiita east coast sasa itakuwa vipi?Mfano watangazaji wa clouds VIVIAN,SKILLS,VENTURE Wote wamejikuta wakiangukia humo humo sasa wakikaa kwenye kipindi si wanajifagilia tu watu wengine wanabaniwa halafu kuna kamtindo watangazaji wa clouds wameanzisha eti kabla ya nyimbo yoyote ya msanii wa upanga ikitaka kupigwa wanaweka promo ya mwana FA aliyotumia bit ya NI RAHA TU Halafu ndo nyimbo iafuata,Mi naona huko mbeleni tunapoelekea kuna kitu tu kitatokea,sijui tupo!
mkuki
Junior Member
Posts:28
Joined:Thu Nov 09, 2000 8:01 am
Contact:

Fri Sep 12, 2003 7:36 pm

ODB hiyo mwanangu itatokea tu maana kila mahali ni hivyo hivyo tu promo zinaanzia kwenye redio na madj wa club na hapo ni kama unawajua au kuna kitu wanapata kutoka kwako...kuwa Rapper sio kuimba tu inahitaji ujue pia industry inapelekwa vipi? Na kwa bongo promotion kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kwa redio na sijui sasa hivi nadhani pia clubs kwa hiyo ukiwa mjanja inatakiwa uwe una establish relationship na hao jamaa ili upae rotation. Kwa wale ambao wanaiangalia hiphop kama means ya kutengeneza mshiko ndio inabidi wafuate hii model (lazima utoe hela ili kupata hela...si ndio rule ya commercialism hiyo? na kama wewe ni commercial rapper ndio inabidi ucheze by the rules!)

Kwa wale Ma MC wa kweli ambao wanafanya sanaa kwanza kabla ya hela hao ndio inabidi wawe radical...hii ni pamoja na self promotion kama kuuza tapes kutoka kwenye buti ya gari, website, na kadhalika...lakini kwa hawa marketing sio muhimu kama skillz zako...hiyo ndio biggest marketing tool. Nchi yenyewe ndogo bongo sio kama Marekani ambapo ni size ya bara kwa hiyo kusikika kama una kichwa kilichotulia na unajua what to do basi unaweza kupata exposure. Option nyingine ni kuanzisha label yako mwenyewe na watu kama wewe ambapo mtakuwa mnasaidiana kuinuana wenyewe kwa wenyewe. Hao East Coast na Walumendago wanachofanya ni kama Semi-label yaani colabo mnafanya pamoja na kadhalika hii ipo kila mahali...kuanzia akina WU-Tang mpaka St. Lunatics (From real tu not-so-real!) hii inasaidia kuwa na identity fulani ambayo inasaidia mauzo, ni kama logo vile maana ukisikia sound fulani au style fulani unajua hawa watu fulani halafu kila mtu anamfagilia mwenzake mwishowe kila mtu anakuwa anachangia washabiki kitu ambacho kinaongeza mauzo kwa kila mmoja. Kwa hiyo mwana ingawa hata mimi simaindi huku kujifanya wamarekani wamarekani lakini hii haiendi popote kujua kupo kila mahali inabidi tu uwe mjanja ili kulicheza game ipasavyo
ODB
Junior Member
Posts:37
Joined:Fri Nov 23, 2001 8:01 am
Contact:

Sat Jan 17, 2004 12:32 pm

Hey mazee! happy new year!

Nadhani si peke yangu wala si peke yako unayekerwa na core hii ya kisenge,nadhani hata wasanii wenyewe wameshavumilia na wamechoka mmoja wapo ni mzee wa MTAZAMO a.k.a MZUNGU WA ROHO-AFANDE SELE

nadhani mmesikia wenyewe anavyowapaka watoto wa upanga ama kweli NI DARUBINI KALI-nasema hivi kwani ni wachache ndo wanaweza kumuelewa na waliopakwa ni kama ifuatavyo.

Mfano:-Nyimbo zima imejaa majina halafu haina vina

Hapa anapakwa GK na wimbo wake wa TUPO PAMOJA

Mfano:-kuna tofauti gani kati ya masaki na mbezi ni sawa kuvaa blanketi miguu inangatwa na mbu

Hapa anapakwa GK tena akimaanisha kunatofauti gani kati temeke na upanga

Mfano:-Unaimba nyimbo za sherehe kila siku wakati vijijini watu wanakufa kwa njaa

Hapa anapakwa AY "mzee wa comercial"kwani nyimbo zake zimebase kwenye raha kama vile NI RAHA TU,NIRAHA TU REMIX,RAHA KAMILI,RAHA KAMILI REMIX Unaweza kuona takribani ni nyimbo nne zinaelezea raha wakati kijijini watu wanakufa kwa njaa

Mfano:-Unasifia ngono na mademu kijana vipi!

Hapa anapakwa O-ten na wimbo wake wa NICHEKI anaposema

" NAPENDA SANA POMBE NAPENDA SANA MADEMU KIFUPI NI STAREHE"

Vile vile kapakwa mwana Fa kwa kuwafagilia mabinti nadhani mwana FA kashtuka na keshajitoka kwa habari nilizozipata.

BIG UP AFANDE SELE nadhani ni changamoto nzuri sana kwa wasanii wa bongo ila mwanangu kaua

mfano:-Unaimba nyimbo za mapenzi na unaishi kwenye jumba la udongo nadhani message sent!

Ni kweli hip sio kama siasa za bongo na kwenda mtoni si kama unakwenda kwa sir GOD

hiyo ndo darubini!
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 3 guests