Kora Awards 2002

Moderator:Juma4admin

bongonian
Junior Member
Posts:15
Joined:Sat Nov 03, 2001 8:01 am
Contact:

Tue Aug 20, 2002 7:30 pm

kwa kweli inatiauchungu kuona hiyo kora kila mwaka hatujawihi kutoa mshiriki (nominee) hata mmoja ingawa sina uhakika na staili yao ya kuchagua hao washiriki sema niliwahi kusikia msanii anatakiwa apeleke kazi yake kitu ambacho kama ni kweli basi itakuwa ngumu kupata wshindi wa kweli si kwa africa mashariki tu bali nadhani kwa africa nzima.

pia hiyo kora kwa aina fulani inamapungufu mengi tu kwa upande wangu ..kwani kama ni ya africa inakuwaje hakuna nchi nyingine inayopewa nafasi ya kuyaanda zaidi ya sauzi africa au sauzi ndio africa yenyewe...

pili kwenye swala la watumbuizaji ..mimi kama ningetegemea wasanii wa africa wangepewa nafasi kubwa katika utumbuizaji kwenye ile siku yenyewe ya kutoa zawadi kwani ndio siku ambayo watu wengi wanaangalia zaidi ya ile siku moja kabla ya utoaji tunzo kama walivyofanyiwa akina JD....kwani siku ya tunzo zenyewe wanaoja kwenye utmbuizaji ni wasanii wengi kutoka africa kiasi kwamba hata hao wa kwetu wanafunikwa.

Nadhani Kora ingeangaliwa upya kwa ujumla ili kiwe kioo cha kutangaza muziki wa africa
bongonian
Junior Member
Posts:15
Joined:Sat Nov 03, 2001 8:01 am
Contact:

Wed Aug 28, 2002 12:09 pm

oya kisiwa nimekuelewa pale unaposema wasanii wetu hawajitangazi sana nje ya bongo lakini pia kwa upande fulani sasa hivi nyimbo zao zinajitahidi kusikika hata nje ya bongo siunaelewa tekelinalokujia (technolojia) ...hilo swala la kujitangaza kimataifa nadhani lilishawahi kuzungumziwa kipindi cha nyuma na utaona kuna uzembe wa wasanii na pia vikwazo ambavyo vinakuwa ni vigumu kwa wasanii wenyewe kuvivuka.

turudi kwenye sehemu ya kora kufanyika.....nadhani waandaaji walipofikiria swala la kora walijua hali halisi ya africa kwani wao pia ni waafrika walio afrika ...hivyo sitegemei hicho ndio kigezo cha kuweka tamasha hili Sauzi kila mwaka....nia m\ni kutangaza na kuwatunza wasanii na kazi zao sio siasa ya ...kwani kama unafahamu vizuri hiyo sauzi inaweza kuwa kati ya nchi zilizoendelea sana afrika na pia ni moja ya nchi zilizo na umaskini wa kutupwa afrika...... kumbuka hizo awards zinafanyika ndani ya ukumbi sio barabarani hivyo hata hapo tanzania inaweza kuwa waandaaji kama kukiwa na fungu la maandalizi kutoka huko kora.
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 10 guests