MTU WA KWELI

Moderator:Juma4admin

Mchapakazi
Member
Posts:86
Joined:Thu Mar 01, 2001 8:01 am
Contact:

Thu Apr 28, 2005 5:00 pm

mueleze atambue kwamba hip hop kazi/

ajitaidi kupanda ngazi kwa ngazi/

sio kurukia tu asije pata razi/

na misingi ni vina, mashairi pamoja na mavazi/*

usije kujaza shazi/ na kushusha hadhi/

hii forum na ya wanahip hop sio mabazazi/

angalia Sky kuna tofauti kati ya dafu na nazi/*

we si msanii ni paparazi/

hata kwenye lines tunaweza kubig up kwa new Papa Ratz/

kughani kwangu time yoyote hiyo iko wazi/

popote naongoza jahazi toka north mpaka Sauzi/*

Ona sasa umekimbia/ nasikia unalia/

kisa wamekuanzishia gwarida la kushoto kulia/

hii ngome utaadithia/ pia/*

maana fake MC's ndipo walipofia/

kama kiwanja mimi Amsterdam Schipol, wewe Kia/

nakuona unavyoofia/ na ndio maana kila siku unashika mkia/*

Watch ya out Son, I can give lil tip in writing skills, holla....
skywalker
Junior Member
Posts:35
Joined:Tue Apr 05, 2005 8:33 pm
Contact:

Sat Apr 30, 2005 8:53 pm

Ilikuwa ni likizo tyme nikila happy na shemeji yenu/

so im back turhyme tugongenishe zangu na zenu/

4 REAL nawakilisha hippop tofauti na yenu mayenu/

AU muziki fulani wa huko kwa kina iwe mbwenu/

sijakimbia niko stead kama Al-zarkawi/

mi ndo mti bwana washamba bakieni matawi/

rap si tunguri madogo siamini uchawi/

Is all about talent iwe bongo hata malawi/

nafunika kwa fujo najua mlidhani hayawi/

Nicheki niko tîght mazeee ebana eeeee/

narule kwa stye aisee ova kamikazeee/

starling kwenye movie,nafight mtoke ushuzi/

pruuu :lol: kama kazi roba za mbao ustaadh.........

im still blazing...........an welcomin you kids
Knifebutcher
Member
Posts:112
Joined:Wed Nov 12, 2003 4:27 pm
Contact:

Sun May 01, 2005 2:27 pm

nacross kama kete lazima unicrown ukingi

kama rymes ni shule we bado uko msingi

kama ni umri basi we unatambaa na mimi ni dingi

kivipi unajaribu kupambana na vigingi

kigezo cha uemcii sio kuwa na miverse mingi

lakini we poyoyo mpaka mida hii hujanielewa

ngoja nianzee kukuburuza kama behewa

nitakuacha ussafocate kwa kukosa hewa

hapa ni mchaka mchaka tuu yaani kindewa ndewa

oya we dogo wa musoma huchikii wewe :evil: :evil:
quertzal
Junior Member
Posts:49
Joined:Fri Feb 11, 2005 3:57 pm
Contact:

Tue May 10, 2005 5:08 pm

Vipi kijana sky mbona sana midomo unachonga//

huna mpya naona kwa wanaume sasa wajigonga//

ni quertzal kidume wewe hapa ni shoga//

husije kwa woga na meno kuchonga hapa utafanywa boga//

hivi ni wewe kijiba fyuzi mtoto wa juzi juzi//

uliyepata tuu ni simulizi za wakufunzi wa hili kulunzi//

twende kazi kama unajua ku-kwea mnazi//

hili ni nyundo la kijambazi kaa wazi nikupe kazi//

husipende siasa wakati hauna darasa//

sawa kupenda anasa na kelele wakati huna kinasa//

huna thamani na karata yako garasa//

wee we wee weee kaa kimya tena fyata mkia//

tunapopita amkia huna sifa utakula vilivyo bakia//

unajaribu tunisha msuli kwa ugali kiporo na dagaa mbili//

unakuja umevaa msuli na kutunisha zako mbavu mbili//

kijana mdogo mvua mawingu yake dalili//

hapa tutakupembua tukubakizie punje mbili//

karibu dsm tufunze japo kiswahili//

utapate sema nasi tukusajili//
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 1 guest