MTU WA KWELI

Moderator:Juma4admin

quertzal
Junior Member
Posts:49
Joined:Fri Feb 11, 2005 3:57 pm
Contact:

Fri Apr 15, 2005 1:54 pm

Sikai meza moja na wanafiki/wanakenua meno ujue marafiki/dhiki zimewajaa nyoyo zimesheheni chuki/wanaoneaka smart kumbe nyuma wameficha bunduki/mc sasa ngangari mwanzo mpaka mwisho wa week/nimekuwa mtu wa kweli/yaani natumia akili maarifa yakizidi mwili/ nabadilisha nyendo bila kupoteza asili/ ujuzi na mbinu zangu zanifanya jasiri/kama unata battle tukutane wawili na siku tam ni jumapili/ hapa nipo kwa wito na si kufuata ujiko/nang'arisha popote mlipo baharini mito mpaka vijito/rhymez zina mvuto usafiri wangu bito kamwe si vunji miiko na mziki wangu mzito/ sipendi propaganda enyi nyote nawasabai/ sitaki makuu napanda Punda ili wa chini niwape hi/ nakata ngebe kimtindo midoshoo nawapa dry//siitaji nguvu ya kilevi/ ili kwenye stage nionekane heavy/si chagui sibagui nitawarusha wenye jealous na envy/mc nang'ara mashariki ya mbali mpaka kimara/ si chagui biashara/ sitaki ujiko kwenye radio uchwara/Big up knifebutcher waelimishe uku ukiwarusha/salaam Alcapaino battle zako hazina mfanooo

Lyrica Blower!

Quertzal
skywalker
Junior Member
Posts:35
Joined:Tue Apr 05, 2005 8:33 pm
Contact:

Sun Apr 17, 2005 2:23 pm

Amani tena hakuna mbabe anapovuma/

MC mwenye nguvu usoni kavaa chuma/

Kwa mtindo braza utazidi kubaki nyuma/

Kupisha ndo utapisha simba akiunguruma/

Rhymes zako kinda,kama mtoto we kitinda mimba/

Usisite kuniamkia ukipenda niite mjomba/

Ukitaka we nifuate bure kurap ujifunze/

Kama hunijui mi ndo sky,mc natamba hewani/

Karibu kwenye mkondo najongea nishike chati::::::
quertzal
Junior Member
Posts:49
Joined:Fri Feb 11, 2005 3:57 pm
Contact:

Wed Apr 20, 2005 5:24 pm

Watu wa mjini ndio wa kwanza kuliona jua//

nafikiri hili wewe bwana mdogo wa bush bado tambua//

na ni sisi tunawakilisha na kufanya nyinyi ki-mc mpate kukua//

sasa unatukana wakunga je hiyo mimba utajifungua??//

hichi kichwa kimejaa thawabu na hekima za ki-mababu//

uki-battle babu hapa aibuuu na maisha yako ki-mc yatakuwa ya taaaabu//

naona unajaribu traatiibu kukwea merikebu iliyojaa waarabu//

mikono yako laini utaishia chezea tuu zangu sharubu//nitakupa hifadhi na moja ya vazi lako binti skywalker itakuwa ijabu//

natumia nguzo na itikadi zenye misimamo//si fanyi tuu vijimambo watu kama nyinyi mpate msemo//natoa ujuzi ikibidi niletee demo//

nabadilika kutokana na mingi yangu ya maisha mifumo//najua huwezi kujifunza bila kuchafuka njoo hapa nitakuogesha kwa omo//mimi ni sebby a.ka. quertzal mind blower//mbona huna hema si ulikuja moto hapa umepoaa//nimekata yako kauli nimekuacha unakoa//

quertzal n knifebutcher ndio wazee saluti mpaka kwa machangu doa//

kama kawa//

Mind blower//

Quertzal//
skywalker
Junior Member
Posts:35
Joined:Tue Apr 05, 2005 8:33 pm
Contact:

Thu Apr 21, 2005 7:43 am

Bila shaka bwan'mdogo unaiamini methali hii ya chini/

Kwamba jogoo la shamba haliwiki mjini/

Nataka nioneshe mapinduzi makali kiasi usiamini/

Umemchokoza mbogo lindoni,Ingekuwa vema ukakaa kibindoni/

Kamwe sitapata huruma kukufukia shimoni/

Umeyavulia mweyewe maji sharti uyaoge bafuni/

Mi ndo sky kama msunni naingia vitani/

Ninapochokozwa kamwe dunia haina amani/

Eti sebby wa kimara unataka yangu nishani/

Au nikupe box ya mdomo utokee dirishani/

Pengine nitoe mahari nikuokoe maishani/

Wapendeza binti kijana eti we kabila gani/

Mi kwetu kukatana mapanga si jambo geni asilani/

Nashangaa mtoto wa mama unanilazimisha niingie hasirani/

Ni bora mwenzio knife bucha ukweli ameubaini/

Kafyata mkia, na heshima utadhani kawekewa plasta mdomoni/

We ndo bado naandaa dawa yako jikoni/

rhymes ndo silaha harafu ndo hivyo ziko pomoni/

Angalia kwenye battle za lugha ya kimombo/

Uone jinsi sky nilivyoinyanyua Bongo/

Nimekomaa na machizi wa huko ng'ambo/

Na sasa P kubwa, wamegundua kuwa mi ndo mtambo/

Kwanini hunipi heshima mimi kaka yako/

Nikufundishe kuimba rap uwashinde adui zako/

Any mshikaji waingereza husema:OPPORTUNITY COMES ONCE IN LIFE TIMES,mimi nishazeeka mdogo wangu, tumia muda huu nikurithishe mikoba ya sanaa utoke mpaka lini utaka unakomaaa,Aiseee unachekesha.teeeeeh..teeeeeeeeeeeeeeh.
quertzal
Junior Member
Posts:49
Joined:Fri Feb 11, 2005 3:57 pm
Contact:

Thu Apr 21, 2005 2:05 pm

Bwana mdogo hii tsunami//unataka kuburuzwa chogo hii kambi ya army//

naona unatema fyongo huyu ni quertzal 120 hata kona za mto wami//

rudisha kikosi nyuma pindi pale upepo wangu unapo vuma//

huwa sina huruma/nachakaza kizazi chenu maendeleo narudisha nyuma//

unacheza na nyati wakati hauna shati//ni sawa kupiga kelele jukwani bila kipaza sauti//ukija mjini njoo smart lakini husi chomekee suti//jipulizie perfum husije unanuka hudi//umepita mtaa wa magaidi/utachokozwa ikibidi hata kwa maksudi//wewe ni kinyama cha mwitu halali ya mafisadi/

kama unapenda beef qurtzal hapa sheriff//kama unataka utiifu hiki kichwa cha chief//si pendi vita na wenye game dhaifu//uwa nazoa point bila kufika uwanja wa beef// nina jeshi zaidi ya siafu sijali wewe ni mwana ccm au cuf//inavutia mc wa musoma mtandao unapokuunganisha na sisi watu wa dunia//bado kitu kimoja rhymes zako hazija simama hilo staacha kukuambia//anyway keep hooked na mazoezi mengi yatakuinua//hii ndioo dunia quertzal 4life AMINIAAAAAAAAA!!!!!

Mind blower!!

Quertzal!!

Knifebutcher yupo kiwanja mara moja hata kwenye ndoto atakuzukia don worry keep cloz to ur short.
skywalker
Junior Member
Posts:35
Joined:Tue Apr 05, 2005 8:33 pm
Contact:

Fri Apr 22, 2005 7:35 am

Qurtazal mdogo wangu hivi huogopi moto wa gesi/

Au tu unamind kaka yako nishikiliwe kwa kesi/

Ungekuwa unajua ungeufunika mdomo wako upesi/

Mi ndo stone cold nashangaa unaleta kibesi/

Kama game ni hospitali mi ni Dokta we ni nesi/

Mbona hunyamazi wakati unajua i'm expected no mercy/

Umesema umekodi jeshi harafu unamleta huyo kibonde/

Usikonde,mtu single kama tangawizi mi niwaponde/

Nakushangaa sana mdogo sebby,umekodi mwimbaji au mchemkaji/

Juzi katoka nursery ati naye a-battle na mf***ji/

Hapa no stop,mashambulizi mpaka uzeeni/

Na rise to the stop,wachovu wachovu njia iachieni/

Navaa nguo za cop,watuhumiwa nyie sambaeni/

Si bongo flava ni kwa rap,najaa ulingoni/

Na hizi rhymes na zidrop,mpaka masikioni/

Eyo eyo navyo blaze,wachovu hatiani/

Sifanyi mchezo na wash**zi,wasio makini/

Hebu kamata kisha nata na mkia fyata/

Sifanyi battle na msanii anaeng'ata/

Wenye akili wamejitoa na hili sakata/

Wameshahisi moto mkali ujinga wameachaaaa..

Hey little boy, u better warn dat Bitch,before I break his mouth,Im not as simple as he thinks I might be,tell him fu** off.
Mchapakazi
Member
Posts:86
Joined:Thu Mar 01, 2001 8:01 am
Contact:

Mon Apr 25, 2005 10:49 am

Hakuna kitu kamwe uwezi kuwa emcee wa kudumu/

mchovu kimashairi kama mgonjwa wa pumu/

I treat ya like mchumba nunu/

nakupa kichapo alafu kama Ali Chemical nakumwagia silaha za sumu/*

ati ng'ambo ass whole unakaa Tarime au Mugumu?/

alafu unaingia ovyo anga za wagumu/

nitakujaza mashairi waungwana wakuhukumu/*

Kwenye L waweka R na R waweka L lini kiswahili kimekua lugha ngumu?/

ushamba umekuganda brother tena wa kudumu/

lete bia mbili ushakuwa kama simba wa bar muhudumu/

tunapoteza wajinga kama nyie ili hip hop idumu/*

nasikia huko gongo kwa vidumu/ hali ya maisha ngumu/

utaweza wapi kusplit wakati daily wanywa chi/kimpumu/*

heri ndumu/

so Son watch ya steps this is more official punk....../*
skywalker
Junior Member
Posts:35
Joined:Tue Apr 05, 2005 8:33 pm
Contact:

Tue Apr 26, 2005 12:35 pm

84 ndo umezaliwa wakati sky std seven ndo nahitimu/

Huoni tofauti kubwa kati ya chungwa na ndimu/

Tanzania watoka sehemu gani Muleba ama kamachumu/

Mbona adabu huna unaropoka kama binti fulani aitwa kuruthumu/

Pengine tukupe sketi ubadili jina uitwe mwatumu/

Toka ujue kuvaa chachacha kaunda suti na njumu/

Hutaki kabisaa kuambiwa mitkasi fulani ya muhimu/

YAH ni kweli life la huku mjomba watoto walegevu haliwafai/

Wewe na mabishoo wenzako mlozea asubuhi tu chai/

Nivigumu kustahimili labda mahardcore akina Sky/

Watu wa huku wamepinda hawafagilii kabisa maspy/

Whatch out kid.......
Mchapakazi
Member
Posts:86
Joined:Thu Mar 01, 2001 8:01 am
Contact:

Wed Apr 27, 2005 9:17 am

Yoh Yoh one two three to da four/

asubuhi ya J4/ nashusha free flow/

najua uwezi maana we bishoo/

we I do ma show/ for u is big blow/

niko makini kama GURU au Curtis blow/

vina bora vitavyokuamisha ulipo kuja kariakoo/

mjomba hapa ni so/

najua nimekukaba koo/

na sasa naona unasound down low/

hamia kidali poa/ hama promo za ukimwi na wala usione soo/

nilikuwa Compton na NWA the yr ya mention, yeah it was eighty four/

hivyo hapa sky punguza mapepe na uje slow/

maana kama life tough hivyo, that means u don't have dough/

jitaidi kuuwa soo/ bongo yako hiyo, usije osha choo/

kaza kaza basi hata kwa siku online mara moja njoo/

Reply unipe hamasa/ kaka

nikupe mashairi ya kutakata/

yakuoshe kuliko sadaka/

maana robo tatu unaflow taka/

that's tru kaka/ usije sema napaka/

kama umenunu sema nyau kama pakaIMAO
quertzal
Junior Member
Posts:49
Joined:Fri Feb 11, 2005 3:57 pm
Contact:

Thu Apr 28, 2005 3:53 pm

Nimeshakuteka bwana mdogo kama ibilisi//

akili, fikra,mawazo yako quertzal amefilisi//

haufai kuguswa umesheheni nuksi// hichi kichwa kiite quertzal a.k.a kamusi//

huna ladha,thamani,damu ilishanyonywa na quertzal chunusi//

mjane skywalker umebaki msusi//

umiza kichwa,natuliza akili kama unacheza chess//

kidaraja niite askofu wewe bado shemasi//

huna pa kujibanza ki-mistari sebby nasaza//

ki -hiphop ushachakazwa quertzal kote nameza//

huna nafasi mjomba iliyobaki ya mke wenza//

ushazoea kuoga porini wapi utaweza jaquuz??//

hili jiji kila cku lakupa njozi tak care utapata uchizi//

haya nayaweka wazi kijakazi husipate simanzi//

dawa si fumanizi wala irizi ujibu quiz//

unacheza na wachapakazi/ kwa chai ya rangi na moja andazi??//

hizi style kamakazi zakupa njoozi//

zikikutafuna ki-mapozi na zikikuchapakazi//

Mind Blower!

Quertzal.
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: Bing [Bot], Google [Bot] and 9 guests