TUNAELEWA VIPI HIPHOP KAMA UTAMDUNI.

Moderator:Juma4admin

tulanongo
Junior Member
Posts:2
Joined:Fri Jun 11, 2004 8:10 pm
Contact:

Fri Jun 11, 2004 9:21 pm

Hayoo ndiyo mambo.. Kwanza kabisaa nashukuru kuona vile vichwa Halisi vya hiphop kujitokeza katika mswaada huu, nimefurahi kuona Hiphop kama KBC kushirikiana nasi katika ile dhamira ya UJENZI, Pongeze sana kwa hilo na tunahitaji watu zaidi, hususani Wakongwe kama nyinyi katika tamaduni hii ya hiphop.

Pia ningependa kuwashukuru ndugu zangu wote mliongia na kutoa maoni yenu, nawaita ndugu maana naamini wote nyie ni Hiphop. Sikunne Saanne na GR8Kwanzini shukurani zangu ziwafikie, hili jina la siku nne saa nne nimejaribu kulitafakari kwa haraka naona napata Jibu la Mkongwe fulani wa sanaa hii [Hizi ni zile Metaphor alizozitaja Mgeni Bahati tena hii ni ya hali ya juu] sasa sijui kama ndiye yule nayemfahamu mimi ama lah, kama ni wewe na amini unanifahamu, basi nifahamishi tuu km ni wewe, naona mzee ungali bado unaendeleza Ubunifu ambao kwa mimi niliyewahi kukutana nawe mara chache falagha ningependa jamii iige au ijufunze katika yale uliojaaliwa na Muumba. Laiti kama ndiye basi mada imepata watu wake.

Haya jamaa, ningependa tuu niwakumbushe pia, kuwa MUZIKI wa RAP ni sehemu tuu ya Tamaduni hii ya Hiphop, naona wengi mmelalia kwenye Muziki ambako ndiye kwenye KERO nyingi kulingana na zile sehemu nyingine, hilo silikatai na nadhani hili ni pana zaidi na nakubalina nanyi kabisaa kwamba sehemu kubwa iliyoathirika na yenye kuhitaji kuhimarika ni hapa kwenye muziki ambapo ndiyo kama MEDIA yetu kama alivyosema GR8Kwanzini, ila ningependa kuwakumbusha tuziguse na zile anga nyingine pia.

KBC naona umemuita Ra, Jina nadhani ndilo RHYMSON analitumia, pia nitafurahi kumuona akijumuika hapa, huku Bongo tumebahatika kusikia baadhi ya nyimbo zake zilizomo ndani ya Santuri yake ya JICHO LAKE, binafsi nampa pongezi sanaa, na hapa naweza kusema kweli MEDIA zinapaswa kupewa lawama, ufanisi alioonesha katika TENZI zake Binafsi ulinigusa sana, na hii inanifanya nizidi kuamini ni bado sana kwa wasanii wapya kuichukua ile heshima ya KWANZA UNIT. Ndani ya zile nyimbo mbili za utambulisho kuna balaa kubwa ambalo nakiri kusema wasanii wa sasa waanapaswa kujifunza mengi kutoka mule, hususani katika kuandaa TENZI ama LYRICS zao. Mshafti kwako Mjeshi Rhymson.

Niliudhunika kusoma Habari zako humu african hiphop bila kusikia zile nyimbo zako, sasa sijui kama zilifika katika Media zetu za hapa Uswazi, hususani kwenye redio.

Katika kutoa kero zangu, mimi naona kwamba Tamaduni yetu hii ya HIPHOP kwa uvivu na ukosefu wa ufahamu ndani ya Media Hususani Radio na Magazeti, wengi wanashabikia zaidi kuandikia na kuzungumza pasi na uelewo juu ya wanachokifanya. Inanikera pia kuona watu wanachanganya BONGO FLEVA na HIPHOP. Nadhani sasa wakati umefika wa kurekebisha jamii. Najua wapo watu kutoka media tofauti tofauti wataanza kufuatilia habari hii, pia ningependa kuwaomba watokapo kusoma habari hii basi wabadili muelekeo wao wa uandishi na utangazaji, na wanapowafanyia mahojiano hao wasanii wawe wadadisi zaidi, ili waweze kutofautisha yupi ni hiphop na yupi ni mbongo fleva na pia waijenge jamii juu ya swala hili na wasitishe upotoshaji.

GR8Kwanzini nakukubalia kama alivyokukubalia KBC kazi hiyo inawezekani iwapo tuu MC hatobadili na madhari ya HIPHOP. Hii ni kazi kubwa ambayo wataarishaji wanapaswa kuifanyia kazi na mambo yakabadilika.

SOKO na MALIPO kwa Rapper yeyote ni swala la kuliweekea Msingi, Ila soko hili linapotafutwa katika misingi ya Kiuvivu na kuipotosha jamii na kuandaa jamii ya Mafuska nahakika baada muda kutakuwa na madhara makubwa mno. Watu wanaimba mambo hata yasiyo fanana na maisha yao, hii inaudhunisha sana, watu wanaimba Mapenzi bila mipaka na Media zinazo tegemewa kueleimisha jamii zinazidunda tuu kwenye masafaa!! Jamani hii tunajenga ama tuna bomoa?.

Mimi nadhani media sasa zinahitaji kubadilika na Ma Dj wao kutimiza wajibu, simulizi za kujenga Hiphop na Jamii zinahitajika kwenye hizi redio [GRIOT] ili muziki upate nafasi ya kujenga jamii. Tunahitaji watu kama akina Kaka Masoud Masoud/ Kunakazi iliwahi kufanywa na KBC pamoja na RHYMSON siwezi kuisahamu, watu kama hawa wanahitajika warudi kufanyakazi na ma mc wabadilike wajijue wao ni nani, MC aliye kamili ni lazima atajihisi yeye kama MJUMBE aliyepaswa kujenga jamii yake. Na si vingine, atuburudishe na kisha atuelimisha.

Uchungu na uzuni niliyo nao siwezi kuumaliza kwa leo hii. Wale wote walio na dhamira ya UJENZI nia ya kuleta UKOMBOZI basi naomba tujumuike uwanjani hapa.

Kila lakheri wakuu!!.
Sikunne-Saanne
Junior Member
Posts:1
Joined:Fri Jun 11, 2004 10:34 pm
Contact:

Sat Jun 12, 2004 1:45 am

Sasa naona hii Mada iliyoanzishwa na bidii kubwa ya bwana Tulanongo inapamba moto sawia.Hii inadhihirisha wazi kwamba wakereketwa wa hii sanaa bado wako hai na tayari kwa mapambano.Hii inanipa furaha kubwa sana moyoni sio utani.Hapa naandika hii wakati Mhandisi wangu wa mitambo ya sauti studio anaandaa mambo tayari kwa recording session ya nguvu usiku wote.Mawazo yenu wanahiphop yatakuwa nami niingiapo kwenye chumba cha vocals na nafikiri siku itafika kazi itakuja kusikika hata kama wenye redio wakifanya njama za kubana.

Nafikiri cha msingi ni kuendeleza tu juhudi. Ni kweli kwamba rap ni kipengele tu kimojawapo na ni sawa kabisa kwamba inafaa tuangaze macho kwa vipengele vyote vilivyopo ndani ya sanaa hii. Dada anayepanga Warsha ya sanaa Arusha nakutakia mafanikio mema sana nafikiri mchango wako ni bora zaidi ya hawa wanaopata majina na ujiko bila kuwa na mapenzi yoyote kwa sanaa hii. Moyo wangu unafurahi sana kusikia kazi za wasanii kama Ra ambao hawafanyi hii kutafuta hela au ujiko bali kwa mapenzi tu ya sanaa. KBC nafurahi kukuona humu ndani maana wewe ndio mkongwe hasaa kwenye hii sanaa.

Bwana Tulanongo kama umeweza kuchambua hili jina na kujua ni nani basi hakuna shaka kwamba upeo wako wa uchambuzi na ufumbuaji mafumbo uko juu sana.Naomba nikupe pongezi kubwa ingawa sina uhakika kama umdhaniaye ndiye. Amani na upendo kwa wote.
Lord Soames
Junior Member
Posts:2
Joined:Fri Jun 11, 2004 7:55 pm
Contact:

Sun Jun 13, 2004 1:23 am

Amani iwe nanyi wapenzi wote wa Hip Hop popote mlipo.

Kwanza ningependa kutoa maoni yangu wa Webmaster/ Designer wa hii website. Ukiandika text yoyote kwenye hii page kisha uka-press Esc kwa bahati mbaya inakuwa umefuta kila kitu. Imenitokea hapa baada ya kuandika maoni yangu kwa zaidi ya 45 minutes, kufumba na kufumbua vyote niliyoyaandika yameyeyuka. Tafadhali rekebisha scripts kwa manufaa ya wengine.

Salam kwa Chief Ismail aliyenidondoshea barua pepe na kunijulisha kuhusu huu mjadala. Nikiwa kama mwana hip hop ni wajibu kuchangia maoni yangu, na hivyo basi yanakuja kama ifuatavyo.

Naona kabla ya yote ni muhimu kukubali kuwa hip hop inakua na kubadilika the world over. Ukiangalia since 1970’s Grand Master Flash, Sugar Hill na wengine walikuwa na style tofauti kabisa kulinganisha na NWA miaka ya 1980’s. MC Hammer and Puffy (Diddy) came along in the 1990’s na kuendeleza mabadiliko hayo, 2000’s kuna kina Nelly, Eve na wengine, history will tell. Kwa mwendo huu naona tukubaliane kuwa kila kitu kinabadilika kufuatana na muda, as much as I DISLIKE bongo flavour, naona nikubali tu kuwa hayo nayo ni mwendelezo wa hayo mabadiliko kama nilivyoeleza.

Hoja nyingine ni kuwa Hip Hop ni UTAMADUNI, na kama ilivyo tamaduni yoyote huwa inakuzwa au kuendelezwa na watu wenye sauti na nafasi (influence) katika jamii husika. Katika jamii ya Hip Hop watu hawa wenye sauti na nafasi ni mapromota (wasiojua/wala kujali nini maana ya Hip Hop), radio Station owners (wanaopenda hela zaidi ya Hip Hop) na radio Dj’s wanaotaka umaarufu kwa ku-support music bila kujali kama ni Hip Hop au Bongo Flavour etc. Hawa ndio watu wanaoshikilia kioo cha Hip Hop katika jamii, bila ya haya makundi kubadilika safari itakuwa ngumu sana.

Solution: Wasanii wa Hip Hop lazima waelimishwe kuhusu hizo Elements 5, wajue kuwa hip hop ni zaidi ya ku-rap na kuvaa jeans kubwa, ni zaidi ya kuvuta bangi, ni zaidi ya kutoa wimbo redioni. Hip Hip ni mimi na wewe kila utakapokuwa kama una jeans over size, unaenda college, una elimisha wadogo zetu kuhusu madhara ya bangi na Aids, unanunua LEGAL copy ya REAL hip hop album, unahudhuria tamasha la REAL hip hop, unatoa maoni yenye nia ya kujenga hip hop, kwenye jumuia za wana hip hop n.k Hiyo ndio Hip Hop. Kama Rhymson na D’Rob (RIP) walivyosema “Sis Wasafiri Bado Tupo Njiani, Sijui lini Tutafika”

Kila la kheri

Lord Soames.
tulanongo
Junior Member
Posts:2
Joined:Fri Jun 11, 2004 8:10 pm
Contact:

Sun Jun 13, 2004 4:44 pm

yeah yeah nimerudi tena..

Lord Soames nimependezwa kuona umetoa maoni yako, mabadiliko yapo katika kila Tamduni, sikatai yatatoke tuu kwa sababu Hiphop inaishi. Lakini Bongo Fleva ni zao jingine tuu la muziki ambalo si Hiphop, Ningependa pia tuzungumzie yaani yale mambo yetu ya Breakdancing, DJing, Beat-boxing, MCing, Graffit Art, Knowledge,Trade na Fashion. Lakini katu tusikubali mabadiliko haya yaondoe mandhari ya Hiphop na kwa mtazamo wangu tuu Bongo Fleva si Hiphop kabisaa, Hiki ni kitu kingine ambacho kimetoke sehemu nyingi duniani. Kwangu naona Bongo Fleva ni kama zao, na kuna kipindi Mkongwe KRS One aliwahi kusema kwamba kufaninisha hiphop na zao ni sawa na Utumwa.. hapa alikuwa akihojiwa na Mhandishi mmoja wa habari anayejulikana kama Nathan RABIN.

Mfano: Tazama pale Pouerto Rico, kwa wasanii wapya kama akina Don Chezan, yeye ameunganisha vionjo tofauti ukiwemo Rap na lakini hapakazii kama anafanya RAP.. na wapo wasanii kama Tego Calderon kutoka kule kule Puerto Rico yeye amechangana salsa na bambo katika Rap zake lakini mazingira ya Hiphop yapo pale pale na kumfanikisha kuuza nakala laki moja ndani ya nchi yake. Pia unaweza kutazama wasanii kama Kwanza Unit walivyofanya katika msafiri nk kama alivyosema KBC na pia tazama kama X-PLASTAZ wanavyo mudu kutengeneza ma mix fulani na kubakisha mazingira ya ki Hiphop kitu amvbacho kimewasaidia kufanya mauzo mpaka nje ya nchi. Kwahiyo naona ni bora kutazama ni mabadiliko gani ya kayakubali na kukataa.

Maoini yangu kwa ma hiphop wote wa Bongo wawe mstari wa mbele kupinga Muziki wa Hiphop kuitwa Bongo Fleva hii ni moja ya vitu vinavyo changia kusahaulika kwa Hiphop ya Tanzania [BONGO].

Watu wa MEDIA wao ndiyo kigezo, laiti kama kweli hiphop wote tunataka mabadiliko basi hakuna budi kubadilika na kufanya mapinduzi kwenye nyanja zote kuanzia pale ulipo., Km wewe ni Hiphop na upo kwenye media jiulize unachangia nini kwenye hiphop.. na kama wewe ni mfanyabiashara jiulize unachangia nini kila mmoja ajiulize kutoka kwa yeye alipo, Hiphop si muziki tuu jamanii jiulize kwanini unapenda Hiphop na una ielewa vipi hiphop.,

Wasanii wa Rap nyinyi sasa ndiyo kama MEDIA hususani kipindi hiki.. na yeyote aliye Hiphop ni lazima ajiulize je mimi naishi kama Hiphop yaani kuanzia kutoa tafsiri na kila kitu : hapa namaanisha kwamba je jikague unaishi vipi na unatoa picha gani kwa watu juu ya tamaduni hii ya Hiphop? Uhuni wako au Busara zako ndizo zina athiri jamii.

Wewe MCee unajua nini juu ya Ume cee au maswala ya ujiko tuu na kujitafutia pesa kwa kuipakazia Hiphop.. Jamani tunapenda wote tuwe Hiphop lakini kama wewe na sisi ma hiphop tunahitaji kuelimishwa na kuburudishwa na muziki wetu lakini siyo kuona leo watoto wetu na wadogo zetu kupotoshwa.. Mtazameni Mzee wetu KK alifanya nini siku ile pale DIMOND JUBilee katika kuchangia mfuko wa chuoo cha kiislamu.. aliimbisha watu I CAN.. Ile ile ya Nas Escoba, yote tuu kwa sababu ya Ujumbe ulikatika nyimbo ile na ndiyo maana kaijua mpaka kuiimba,.

Tunahitaji mabadiliko jamaa la sivyo huko tuendako tutakuja kuona jinsi hii Hiphop itakayo tuadhibu kwa kuto ipa heshima na adhi yake.

Kila lakheri wakuu... na pia wale wenye maoni na kushindwa wanapenda kuzungumza nami faragha basi.. mnaweza kunshushia barua pepe hapa: [email protected] nakaribisha wale tuu wenye dhamira ya UJENZI.

Tulanongo..
gr8kwanzini
Junior Member
Posts:2
Joined:Tue Jun 15, 2004 2:46 am
Contact:

Tue Jun 15, 2004 3:42 am

kbc, umesema kwa uzito sana, yet again.

nadhani tungeanzia kwenye kufafanua chanzo na maana ya hip hop. na kufananisha au kuonyesha kinachotofautisha hip hop na bongo flava. nionavyo mimi ni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana watu wengi, wakiwemo wasanii wanaojiita wana hip hop pale bongo, hawaelewi maana ya mc au anachokifanya kwenye 'context' ya hip hop. inavyoonekana wengi wamo wamo tu kwa ajili ya pesa, kuliko usanii na kundeleza ubunifu wao. yaani hawana la kusema bali wanalopoka lolote lile mradi wana midundo mikali inayovutia (catchy beats and phrases).

pia tusisahau wadhamini au wafadhili, kama ni mwenye studio au kibopa mwenye magoto (nadhani wadosi wadosi wengi wamo kwenye mkumbo huu). wao wanachojali ni kwamba muziki utauzika (au jina lao litatajwa kwenye wimbo au kuweko kwenye cd au cassatte, kama wanavyofanya nchi nyingine). hawajali sana kiwango cha muziki au ufundi wa kutunga. wasanii wengi wapya hawana ile busara ya kusema au kujua kuwa; "if you have nothing to say better to stay quiet than open your mouth to remove all doubt." kwa maneno mengine, kama huna la kusema afadhali ukae kimya kuliko ukifungua mdomo na kubolonga

nina maana ya kusema watu watumie busara ya kuzaliwa na kuelewa kuwa maji yameshawazidi kina. lakini kutokana na mafanikio wanayopata watunzi, hata wasio kipaji, wengi wanaamini kuwa na wao wanaweza kusimama ulingoni na makabambe wengine - kama kina ra (gwiji wa kwanza unit) na wengineo waliokomaa.

kbc na tulanongo naona mnaelewa sana nini kinachoendelea katika hii fani. ombi langu ni kwamba shikeni mwenge juu sana ili wengine pia waone kwa upeo. au vipi? rhymson niko naye sana kwa hiyo nazijua kazi zake na jinsi alivyogangamaa kimsimamo. kweli, ra, ungeingia hapa utoe mawili au matatu ya busara. nadhani ili kuendeleza zaidi hii fani ni lazima kuwa na upeo na kina cha fikra, kitu ambacho kwanza unit walionyesha kuwa nacho. walikuwa ni visionary au walioona mbali na kufungua milango ambayo wengi hivi sasa wanaingia na kutoka bila kujua jasho lililotiririka hadi kufikia hatua hii.

kisha nadhani hivi sasa muziki huu umefikia hatua ambayo litakuwa kosa kutengenisha usanii na biashara (business aspect) ya hip hop. nadhani ili msanii afanikiwe kutokana na jasho lake na ubabe wake wa utunzi, ni lazima uelewe jinsi gani ya kumiliki matunda ya ubunifu wako. nadhani hii itapunguza nafasi ya washashi wanaojifanya ma-promoter na wenye nia ya kusaida wasanii kumbe wanadokoa dokoa kwa faida yao bila ya kujali wasanii na njaa zao (starving artists) kuweka mirija. hata kama wengine watafaidika kutokana na usanii wako lakini isiwe kiasi kwamba msanii anakufa na njaa wakati wasiojua chochote, ila kuwa na visenti tu, ndiyo wanazidi kuvimba kwa uchu wao.

mwendo bado mrefu.
Lord Soames
Junior Member
Posts:2
Joined:Fri Jun 11, 2004 7:55 pm
Contact:

Tue Jun 15, 2004 5:52 pm

OK,

Let’s Rewind.

Hip Hop: 5 Elements, what are they and what do they involve?

Back in '98 KBC and Chief Rhymson had a tutorial on radio 1, back then with Dj Mike Mhagama. They went through these 5 Elements which helped to shed some light into many hip hop heads at that time.

I think it will be a good idea if we could turn this debate into another tutorial of similar kind. Many Hip Hop heads of the moment don't know what these Elements involve and so we can't blame them for calling Hip Hop, Bongo Flavour!!

Knowledge is the key, let’s just put some names of the books, websites, magazines, videos tapes etc that one can go and do their own reading.

Hip Hop 4 ever.
Manyotto Ndimbo
Junior Member
Posts:3
Joined:Wed Jun 16, 2004 8:38 am
Contact:

Wed Jun 16, 2004 8:51 am

Hongera kwa mijadala hii.Nna machache nataka kuchangia vichwa, sasa ntarudi tena kutoa nasaha zangu kuhusu huu UJENZI. Napenda tu kusema inabidi kuweka mikakati ya vitendo ili kufanya mabadiliko yoyote..Ubao huu ama hali ya teknolojia sasa inaruhusu kuanza HARAKATI za nguvu bila watu kuwepo kwenye chumba kimoja. Nikirudi ntaweka sera zangu wazi..Binafsi mimi hupenda vitendo kuambatana na maneno, asanteni wote.

Manyotto Ndimbo
Post Reply
  • Information
  • Who is online

    Users browsing this forum: No registered users and 6 guests